.

.

11 Februari 2016

MUGABE: AFRIKA INAWEZA KUJITOA UMOJA WA MATAIFA!!!


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alisisitiza jumatano kuwa bara la Afrika linaweza kujiondoa kutoka kwa Umoja wa Mataifa iwapo mahitaji yao ya kupewa viti vya kudumu katika baraza hilo la usalama hayatasikizwa.
Akizungumza wa wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika ili kumpongeza kwa mafanikio yake katika kipindi chake cha utawala kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka wa 2015,Mugabe alisema kuwa bara la Afrika limechoka kudhoofishwa na baraza hilo la usalama.
"Nilisema katika hotuba yangu kama mwenyekiti anayemaliza kipindi chake cha utawala cha Umoja wa Afrika mwezi wa Januari, kwamba wakati umefika sisi wanachama wa bara la Afrika kuwaambia wazungu tunaweza kujiondoa na kuunda shirika lingine,"Mugabe alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni