Kiungo Haruma Moshi Boban
atalazimika kusubiri mpaka March 14 kuingia tena kwenye kikosi cha City
kufuatia kusumbuliwa na maralia jambo linalomfanya kuukosa mchezo wa ligi kuu
ya soka Tanzania bara dhidi ya Stand United ya Shainyanga uliopangwa
kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Muda mfupi uliopita mkuu wa kitengo cha
utabibu kwenye kikosi cha City, Dr Joshua Kaseko ameifahamisha
mbeyacityfc.com kuwa mara baada ya kikosi kizima kurejea Mbeya kutoka
jijini Dar kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba, alipata taaraifa ya
kutokuwa katika hali nzuri kwa kiungo huyo na baada ya kumfanyia vipimo
aligundua kuwa Boban ana Maralia.
“Ni wazi hatakuwa sehemua ya mchezo
kesho,ana Maralia tumeshamtaarifu mwalimu juu ya hili na tayari ameanza kufanya
mazoezi maalumu na yule atakayechukua nafasi yake, imani yangu kubwa kuwa
atakuwa sehemu ya kikosi march 14 wakati tutakapokuwa tunacheza na Africans
Sports jijini Tanga alisema.
Katika hatua nyingine Dr Kaseko
alidokeza kuwa kiuongo mwingine wa kati, Kenny Ally Mwambungu ataukosa
mchezo wa kesho kupisha kadi tatu za jano alizopata mfululizo kwenye michezo
mitatu ya City iliyopita, na kukumbumbusha pia kuwa mlinzi Deo Julius
bado atakuwa nje ya kikosi akiendelea kuuguza majeraha ya goti.
“Kwenye mchezo wa kwesho pia tutawakosa Kenny
Ally na Deo Julius kutokana na sababu kadha wa kadha, Kenny amepata kadi tatu
za njano mfululizo kwenye michezo yetu mitatu iliyopita na Deo bado hajapona
majeraha ya goti hivyo nao hawatakuwa sehemu ya mchezo hapo kesho”alimaliza.
City inakutana na Stand United hapo kesho
kwenye uwanja wa Sokoine huu ukiwa ni mchezo wa nne kwa timu hizi huku rekodi
ikionyesha timu hiyo ya Shinyanga kushinda mara mbili na City ikiwa imeshinda
mara moja, hivyo mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na ushindani wa
hali ya juu.
Aliyekuwa mshambuliaji wa City, Paul Nonga
(sasa yupo Yanga) akishangilia mara baada ya kuifungia timu yake bao la pili
kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Stand United msimu uliopita mchezo uliochezwa
kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Chanzo: mbeyacityfc.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni