.

.

01 Aprili 2016

TUKO TAYARI DHIDI YA COASTAL JUMAMOSI


DSC_1254
Kikosi  kamili cha Mbeya City fc,  leo kimeendelea   na mazoezi  kwenye uwanja wa shule ya Sekondari Igawilo kujiweka  tayari kwa mchezo wa  ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga, uliopangwa  kuchezwa  mwishoni mwa juma  hili kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Afisa  habari wa City, Dismas Ten,  ameiambia Mbeyacityfc.com kuwa,  nyota  waliosafiri mikoani kwa mapumziko ya sikukuu ya Pasaka wanataraji  kuungana na wenzao waliosalia  jijini Mbeya  siku ya kesho  tayari wa  mazoezi ya pamoja  kuiwinda timu hiyo  ya Tanga siku ya jumamosi.
Baada ya mchezo wa  Songea  dhidi ya Majimaji, Mwalimu Kinnah  alitoa  siku chache za mapumziko, baadhi ya  wachezaji walisafiri mikoani kuungana na familia  zao, waliobakia  jijini hapa  walianza mazoezi siku ya jana na leo pia  kama unavyowaona, wachache  waliokuwa nje ya jiji  wataungana na  wenzao kesho, hatuna  shaka  yoyote kuhusu Coastal Union na  tuko tayari kwa mchezo wa jumamosi.
Kuhusu  hali za wachezaji wote  Ten  alisema kuwa  mkuu wa kitengo  cha  utabibu, Dr Joshua Kaseko,  amethibitisha kuwa  hakuna  shida yoyote kwa  nyota  waliokuwa wamesalia kambini  wako fiti na wameanza  vizuri mazoezi chini ya Kocha  Kinnah Phiri.
“Nimezugumza na mkuu wa kitengo chetu cha  utabibu na amenihakikishia  kuwa hakuna majeruhi yeyote na  vijana  wako tayri kwa mchezo huku wakiwa na ari kubwa ya kuhakikisha  City inaibuka na ushindi ili  kujiongezea  pointi tatu muhimu na kujiweka  kwenye mazingira  mazuri kwenye msimamo wa ligi” alisema.
Katika hatua nyingine Ten  ameweka  wazi kuwa licha ya Coastal Union kuchungulia shimo, City  haitakuwa na huruma kwenye mchezo huo   kwa sababu  inahitaji ushindi pekee  ili  kupata pointi tatu muhimu zitakazoiweka kwenye nafasi nzuri kwenye  msimamo wa ligi tofauti na sasa  ambapo iko kwenye nafasi ya 13, ikiwa na pointi 24.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni