Mkuu wa Wilaya ya Longido,Mh.Daniel Chongolo (pili kulia) akipata maelezo mafupi kuhusiana na moja ya chanzo cha maji ndani ya wilaya hiyo kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Longido,Mhandisi Musiba
DC Chongolo alielezea changamoto kubwa inayowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo ni uhaba mkubwa uliopo katika wilaya hiyo,pamoja na chanagamoto hiyo kubwa,DC Chongongolo akabainisha kuwa hatua za kukabiliana na uhaba huo zimeanza kuchukuliwa.DC Chongolo akifafanua jambo kwa Injinia Musiba mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo,mara baada ya kufanya ziara fupi ya kutembelea vyanzo vya maji vinavyopatikana ndani ya Wilaya hiyo katika suala zima la kuanza kuchukua hatua madhubuti ya kupapambana changamoto kubwa ya uhaba wa maji ndani ya wilaya hiyo
DC Chongolo akiwa sambamba na Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo Injinia Musiba wakikagua chanzo cha maji kitakachokuwa kikihudumia kata za Tingatinga na Longido kwa asilimia 100.DC Chongolo amesema kuwa Mahitaji ya maji katika kata hizo ni lita za ujazo milioni moja wakati chanzo hicho kitakuwa na uwezo wa kusukuma zaidi ya lita za ujazo milioni 2 kwa siku,amesema kuwa chanzo hicho kipo katika mteremko wa mlima Kilimanjaro wilayani Siha,ambao ni maarufu kwa jina la mto Simba.
DC Mh.Daniel Chongolo (pili kulia) akielekezwa jambo kwa umakini kutoka kwa Injinia Musiba,mara baada ya kuvitembelea vyanzo mbalimbali vya maji vilivyomo katika wilaya ya Longido.
DC Chongolo akiwa na kamati ya ulinzi na Usalama wakikatiza kukagua maeneo mbalimbali yenye vyanzo vya maji,katika suala zima la kupambana na uhaba wa maji uliopo katika wilaya ya Longido,ambayo imeelezwa kuwa ndio changamoto kubwa wilayani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni