.

.

09 Aprili 2015

ALICHOKISEMA 'BIG BOSI' MWAMBUSI BAADA YA SARE NA AZAM FC.





MCHEZO  wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya Azam Fc na City uliopigwa jana Chamanzi Complex Mbagala jijini Dar umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo uliokuwa mzuri na wakuvutia Azam walikuwa  wa kwanza kuleta kashkash kwenye lango la City  baada kipre Balou kupiga mpira mrefu uliotuwa sawia kwenye kichwa cha John Bocco lakini uimara wa kipa Hannington Kalyesubula  aliwafanya wenyeji hao kushindwa kupachika bao.
Dakika kumi baadae City ilijibu mashabulizi kupitia Paul Nonga  aliyefanikiwa kumtoka mlinzi Pascal Wawa lakini mpira alioupiga ulishindwa kulenga lango,  timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hadi dakika 45 za kwanza zinakamilika  hakuna timu iliyofanikiwa kufunga bao.
Azam walikianza kipindi cha pili kwa nguvu hasa kufuatia mabadiliko ya kumtoa John Bocco na kuingia Amri kiemba ambapo dakika ya 61 kipre Balou alifanikiwa kukokota mpira kutoka katikati uwanja na kupiga shuti lilikwenda moja kwa moja wavuni kuiandikia timu yake bao la kuongoza.
Hata hivyo bao hilo halikudumu kwani dakika nne tu baada ya kungia City ilifanikiwa kusawazisha kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Rafael Daud Alfa  baada ya Deus Kaseke kuangushwa kwenye eneo la hatari wakati akijiandaa kupachika bao.
City ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Deus Kaseke na Paul Nonga na nafasi zao kuchukuliwa na Peter Mapunda na Hamad Kibopile mabadiliko ambayo yaliisaidia  kuongeza nguvu ya mashambulizi langoni mwa Azam lakini mpaka dakika 90 zinamalizika  matokeo yalibaki 1-1.
Kocha wa City Juma Mwambusi amewashukuru wachezaji kwa kupambana na kufanikiwa kupata pointi moja kwenye mchezo huo huku akiwataka kujiandaa kwa vita nyingine ya mchezo wa ligi dhidi ya Yanga jumapili ijayo kwenye uwanja wa Taifa.
“Nashukuru mmepambana, tumepata  pointi moja ni jambo zuri kwetu kwa sababu tutakuwa tumesogea kwenye nafasi nyingine, tuna mchezo jumapili hivyo tujiandae  na tujue  kuwa tunatakiwa kuipigania timu yetu mpaka dakika ya mwisho” alisema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni