Jamaa ambaye jina
halikuweza kupatikana mara moja, amejikuta akionja joto ya jiwe baada
ya kudaiwa kukutwa akiiba kwenye shamba la mahindi hivyo kulazimishwa
kula mahindi mabichi.Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni
kwenye Kata ya Miembeni, Bukoba mkoani Kagera na kuibua gumzo kubwa.
Ilielezwa kwamba, katika hali ya kushangaza, kijana huyo hakukataa
wala kuonesha kutetereka kwani alianza kuyala hadi alipoamriwa kuacha
na kuambiwa aondoke.Katika habari hiyo iliyoripotiwa na Mtandao wa
Harakati, kijana huyo alionekana kuwa na matatizo ya kutosikia vizuri
wala kuongea kwa maana ya kuwa ni ‘bubu’.
Hata hivyo, kijana huyo hakujulikana alitokea wapi kwani mbali na
madai ya wizi na ububu pia hakuonekana mwenye ufahamu mzuri kutokana na
mavazi aliyokuwa amevaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni