WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PETER PINDA
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba kutokana na Taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2014/2015 na Mwelekeo kwa Mwaka 2015/2016.
Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mafungu ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka 2015/2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni