Mshambuliaji wa kutumainiwa wa City, Paul Nonga amesema anauhakika asilimia  mia kuwa atakuwa sehemu ya kikosi cha  Mbeya City Fc  msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Akizungumza  mapema leo Nonga amesema kuwa licha ya kuwepo kwa ofa nyingi kutoka timu mbalimbali  zilizokuwa zinahitaji huduma yake  lakini anataka kubaki City kwa sababu ana furaha na maisha kwenye timu hii.
“Ndiyo hata kabla ya msimu  kumalizika kulikuwa na ofa  nyingi kutoka timu mbalimbali ambazo zilionyesha nia ya kutaka huduma yangu,binafsi nshukuru hilo kwa sababu inaonyesha  kazi yangu inakubalika, tayari  nimeshafanya mazungumzo na City na yako sehemu nzuri kifupi hakuna shaka tena juu ya mustakabli wangu ndani ya kikosi,nia yangu ni kubaki hapa kwa misimu mingi zaidi, nina furaha na maisha ya hapa” alisema Nonga.
DSC_0695
Akiendelea zaidi Nonga aliweka wazi kuwa ana shauku kubwa ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara akiwa na kikosi cha City  huku pia akitaka kulifuta deni la michuano ya kimataifa  kwa kikosi hiki anahisi bado anadaiwa.
“Natamani kutwaa ubingwa wa ligi nikiwa na City, hili linawezekana  tumeshiriki ligi misimu miwili kwa mafanikio, nadhani  huu ni wakati wetu sasa imani yangu kubwa timu itakuwa bora zaidi msimu ujao jambo ambalo linanisukuma kuona tunanafasi ya kutwaa ubingwa alisema Nonga.
kuhusu michuano ya kimataifa  Nonga aliyemaliza msimu akiwa amepachika wavuni mabao 4  alisema kuwa bado anahisi deni kubwa  kutoka kwa kwa mashabiki wa City ambao wana kiu kubwa ya kuona timu yao inafungua ramani nyingine kwenye michezo ya kimataifa.
“Nahisi bado ninadeni kubwa kwa mashabiki wa City, ndiyo tumefanya vizuri kwenye ligi  mwa misimu miwili na mashabiki wamekuwa na furaha kwenye hilo lakini bado hatujaka kiu yao ya kushanagilia timu kwenye michuano ya kimataifa  ndiyo maana nataka kubaki hapa ili nilipe deni hilo” alimaliza Nonga.TAARIFA KUTOKA WWW.MBEYACITYFC.COM