Aliyekuwa rais
wa Marekani George HW Bush amelazwa hospitalini baada ya kuvunjika mfupa
wa shingoni alipoanguka nyumbani kwake huko Maine.
Msemaji wake amesema kuwa kwa sasa yuko katika hali nzuri na kwamba kulazwa kwake huenda kukachukua muda mfupi.
Bwana Bush aliye
na ugonjwa wa kutetemeka na hawezi kutumia miguu yake alisheherekea
siku yake za kuzaliwa mwaka uliopita kwa kuruka angani.
Alilazimika kwenda hospitalini mwishoni mwa mwaka uliopita akiwa na tatizo la kupumua.
Msemaji huyo Jim
Grath amesema kuwa Bush huyo ambaye ndiye mkubwa miongoni mwa marasi
wanne wa zamani wa Marekani kutoka familia hiyo atalazimika kuvaa kifaa
cha kuzuia shingo kutokana na kuanguka kwake hapo siku ya jumatano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni