Vijana 30 wa
vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamerudisha
kadi za CCM katika Tawi la chama cha (CHADEMA) Mwananyamala kwa madai
kuwa hawakuridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea wa urais wa CCM.
Vijana hao wa
vyuo vikuu mbalimbali waliokuwa wakiimba wimbo wa tunaimani na Lowassa
wamekabidhi kadi zao za CCM kwa Kaimu Mwenyekiti wa Ofisi ya Mkoa wa
Kinondoni ya Chadema, Bi. Esther Semaja na kukabidhiwa kadi za uanachama
wa CHADEMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni