Ofisi
ya Takukuru mkoani Singida imemuhoji kwa masaa kadhaa naibu waziri wa
fedha na aliye kuwa mbunge wa Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu
Nchemba, kwa tuhuma za kukiuka sheria ya gharama ya uchaguzi na sheria
ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Akiongea
na waandishi wa habari mkuu wa Takukuru mkoani Singida Bwana Joshua
Msuya amesema Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amekiuka sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11/2007 katika zoezi linalo ndelea la kura za
maoni ndini ya vyama vya siasa.
Katika
hatua nyingine Bwana Msuya amewatahadharisha wagombea wote wa ngaza
mbalimbali watakae jihushisha na kutoa rushwa iwe ya fedha au vitu,vifaa
vya michezo, madawati watakuwa wamekiuka sheria ya kuzuia na kupambana
na rushwa namba 11/2007 na sheria ya uchaguzi cap.343 r.e 2002 na pia
sheria ya garama za uchaguzi namba 6/2010.
Katika
jimbo la Singida kaskazini wa tia nia saba ambao wanagombea ubunge kwa
tiketi ya CCM, wametishia kujitoa katika kinyanganyiri hicho kufuatia
msimamizi wa uchaguzi kumwachia mgombea mwenzao ambaye ndiye mbunge wa
jimbo hilo kuto kufuata masharati ya sheria za uchaguzi jambo ambalo
limekuwa kero hadi kutumia vijana wa shule kuonyesha vipeperushi vyake
wakati wa mkutano wa kujinadi.
Kaimu
katibu wa CCM mkoa wa Singida ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mkoa Bwana
Aluu Segamba, amekiri kuwepo kwa matatizo hayo na kuchukuwa jukumu la
kumbadilisha msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na kumweka mwingine.
Baadhi
ya majimbo ya uchaguzi yenye wabunge ambao wameamua kutia nia ya
kugombea tena wamekuwa wakioneka wao ni chanzo kimoja wapo kikubwa cha
kuvunja mashariti ya uchaguzi na kuwasababishia wenzao kuwa na
malalamiko mengi,hadi kufikia hatua ya kuiomba serekali kupeleka maafisa
wa Takukuru na polisi kwenye mikutano ya kujinadi kugombea ubunge.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni