Klabu ya
Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za
Simba 2015 – 2016 kupitia duka la mtandao la Jumia www.jumia.co.tz .
Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora
ya kuweza kununua jezi popote walipo Tanzania.
Kupitia
mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza
upatikanaji wa vifaa vyake ya michezo nchi nzima. Mkataba huu utaongeza
usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba. “Ukuaji kasi wa
upatikanaji wa internet (mtandao) klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa
kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja
wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii ya Jumia – Simba Online
Shop kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba
popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa az Simba kiurahisi na kwa
bei nafuu”. Alisema Ras wa Simba Evans Aveva
Maneja wa
Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul aliongeza kwa kusema
“uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye
maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba. Katika msimu wa 2015 –
2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi
wake kununua jezi za msimu 2015 – 2016 kupitia njia ya mtandao.
Tunajivunia sana kwa Rais wa Simba Evans Aveva kutuchagua Jumia kwa kazi
hii. Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa
wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia Jumatatu tarehe 27 – 7
– 2015 mpaka Alhamisi 31 – 7 – 2015 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya
kuanza rasmi kwa mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa
rasmi kwa rejareja”.
“Tunawahamasisha
wapenzi wa Simab popote walipo Tanzania kuagiza jezi
kupitiawww.jumia.co.tz kuona urahisi katika kufanya manunuzi. Popote
walipo wapenzi wa Simba wanaeza kuagiza jezi kupitia touti ya jumia na
kuletewa mzigo wako mpka mlangoni. Jumia pia inatoa njia tofauti za
ulipia kama ile kuweza kulipia pindi mzigo wakoutakapofika au kufanya
malipo kwa njia za kipesa kupitia simu za mkononi. Kuanzia jumatatu 27 –
7 – 2015 wapenzi wa Simba watapatafursa ya kuagiza jezi
kupitiawww.jumia.co.tz”. Aliongeza Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean
–Philippe Boul.
Kuzungumzia
mapinduzi haya makubwa katika usambazaji wa vifaa ya michezo ya klabu
ya Simba Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited Imani Kajula
ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya
Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba
kuongezamapato yake pia kudhibiti bidhaa feki, kupitia Jumia Online
Shops (duka la mtandao la Jumia) wapenzi wa Simba watanunua bidhaa za
Simba kupitia washirika halali wa uuzaji wa bidhaa za Simba Tanzania.
Chanzo:Shaffihdauda.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni