Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa wameanza kujenga mabanda eneo la Jangwani jijini Dar wakiwa kwenye mabanda yao.
Hiki ni kibao kinachoonesha mpaka wa kufanyia biashara eneo hilo.…
Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa wameanza kujenga mabanda eneo la Jangwani jijini Dar wakiwa kwenye mabanda yao
Hiki ni kibao kinachoonesha mpaka wa kufanyia biashara eneo hilo.
Taswira ya mabanda yaliyojengwa eneo hilo.
Hapa ni kamba zinazoonesha viwanja vya watu kabla ya kuanza kujenga eneo hilo.
Mwenyekiti
wa wafanya biashara ndogondogo, Sadati, Salum Shemboko akionesha bango
la Halimashauri ya Manispaa ya Ilala linalowaonesha mpaka wao.
NI nani
wa kutegua kitendawili cha wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama
‘wamachinga’ juu ya sakata linaloendelea miongoni mwao baina ya Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) la kuwataka
kuondoka eneo la Jangwani walilokuwa wamehamia kwa ajili ya kufanya
biashara zao.
Hali hiyo
imekuja baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia kwa Mkuu wa
Wilaya Ilala, Raymond Mushi, kuwataka wamachinga wa maeneo ya Ilala Boma
na Kariakoo waliokuwa wakitandaza biashara zao chini kuwataka kuhamia
eneo la Jangwani, jambo ambalo sasa limezua patashika.
Akizungumza
na mwandishi wetu, mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo wa eneo la
Jangwani, Sadati Salum Shemboko, amesema kuwa anashangazwa na kauli ya
NEMC kuwazuia kufanya biashara katika maeneo hayo ya Jangwani wakati
wapo pale kwa tamko la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Alisema
kuwa mpaka sasa wametumia gharama nyingi kwa kujenga vibanda sehemu
hiyo na hawaoni watafidiwaje. Alionya kwamba NEMC na Manispaa ya Ilala
wasipokaa pamoja, watasababisha matatizo.
(HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni