Jeshi la Polisi mkoani Iringa limewakamata wahamiaji haramu wanane raia
wa Ethiopia waliokuwa wakisafiri isivyohalali na bila kibali cha kuingia
nchini wakiwa wamepakiwa kwenye gari ya kusafirisha magazeti ya kampuni
ya Mwananchi Communication.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Peter
Kakamba amesema watu hao raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kituo cha
ukaguzi wa magari Igumbilo manispaa ya Iringa wakati jeshi la polisi
mkoani hapa likiwa kwenye operesheni ya kawaida limewakamata raia hao
pamoja na mtu mwingine mmoja anayedaiwa kuwa msindikizaji lakini
haikufahamika kama alikuwa akisindikiza magazeti ama alikuwa
anasindikiza raia hao wa Ethiopia.
Katika tukio lingine kamanda
Kakamba amesema mnamo siku ya tarehe 25 gari lenye namba za usajiri
T.275 BMW lilikuwa likiendeshwa na Manase Alen mwenye umri wa miaka 29
liligongana na pikipiki iliyokuwa imepakia abiria wawili maarufu
mishkaki ambayo haikuweza kufahamika namba zake kutokana na kuharibika
vibaya iliyokuwa ikiendeshwa na Filbert Mmale na kuwaua papo hapo dereva
huyo wa pikipiki na abiria wawili Emmanuel Kitosi miaka 30 na Hamisi
Sigara wote wakazi wa Mseke mkoani Iringa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni