Katika gazeti la
Tanzania Daima ukurasa wa 5, toleo namba 4070 la tarehe 25 Januari,
2016, lilichapisha habari yenye kichwa cha habari Polisi “waisoma”
namba. Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa askari Polisi hivi sasa
wanatakiwa kujilipia gharama za umeme.
Jeshi la Polisi
nchini, linakanusha vikali taarifa hiyo kwamba siyo sahihi. Ukweli ni
kwamba askari polisi wote makambini wanalipiwa umeme na serikali,
ikiwemo wale ambao nyumba zao zimefungiwa luku kama njia ya kuboresha
huduma na matumizi sahihi ya umeme. Baada ya askari kununua umeme
hutakiwa kuwasilisha stakabadhi ya malipo ya umeme kwa ajili ya
kurudishiwa kiasi cha fedha walichonunulia umeme kila mwisho wa mwezi.
Aidha, habari
iliyochapishwa na Tanzania Daima ililenga kupotosha umma na mwandishi wa
habari hiyo hakutafuta ufafanuzi kutoka kwenye mamlaka husika.
Kufuatia hali
hiyo, Jeshi la Polisi nchini, linamtaka mhariri wa gazeti la Tanzania
Daima na waandishi wake wa habari kuwa makini na habari wanazoziandika
hasusani taarifa zinazohusu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuepuka
madhara ya kiusalama yanayoweza kutokea kutokana na habari wanazozitoa
zisizo na usahihi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni