Aliyekuwa spika wa bunge la Botswana, Margaret Nasha amehamia chama cha upinzani,Umbrella for Democratic Change (UDC) kutoka kwa chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP).
Nasha ambaye aliteuliwa mwaka wa 2009 kama spika wa kwanza wa kike alisema kuwa amejiunga na chama cha UDC baada ya kupendezwa na mwelekeo wa chama hicho.
Huku uchaguzi mkuu ukiwa umeratibiwa kufanyika mwaka wa 2019, kampeni
zimeanza huku pande za upinzani na chama tawala vikijitahidi kuimarisha
umaarufu wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni