Mahakama ya
Kimataifa ya Jinai ICC imesema itatoa hukumu dhidi ya Makamu wa Rais wa
zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean-Pierre Bemba
anayekabiliwa na tuhuma za jinai za kivita, tarehe 21 mwezi ujao wa
Machi.
Hukumu dhidi ya
Bemba ni ya kwanza dhidi ya Makamu wa Rais wa zamani katika mahakama
hiyo ya kimataifa iliyobuniwa mwaka 2002 mjini Hague nchini Uholanzi,
ili kukabiliana na makosa ya jinai na haswa ya kivita.
Bemba
anakabiliwa na mashtaka matatu ya jinai za kivita na mawili dhidi ya
binadamu, anayodaiwa kufanya kati ya Oktoba 2002 na Maci 2003 katika
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Makamu wa rais
wa zamani wa DRC anakabiliwa na mashtaka ya kutenda jinai za kivita na
dhidi ya binadamu kwa kuwatuma wapiganaji wa MLC katika Jamhuri ya
Afrika ya Kati mwaka 2003 ili kusaidia kuzima mapinduzi ya kijeshi dhidi
ya rais wa wakati huo, Ange -Felix Patasse.
Hii ni katika
hali ambayo, Umoja wa Afrika AU umepasisha pendekezo la serikali ya
Kenya la kutaka nchi wanachama wake zijiondoe kwenye Mkataba wa Roma,
uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni