.

.

21 Mei 2015

DKT. BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU TATU, NCHINI CHINA,

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, 'Peoples Great Hall' baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China
 CREDIT MJENGWA BLOG

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni