.

.

15 Mei 2015

WAHAMIAJI 600 WAOKOLEWA NA INDONESIA.


Mbeyafm Redio's photo.Zaidi ya wahamiaji mia sita wamewasili katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia baada ya kuokolewa na wavuvi mashua yao ilipokuwa ikizama.
Ripoti zasema kuwa mashua nyingine ilirejeshwa Indonesia na jeshi la wanamaji.
Mwandishi wetu anasema kuwa wengi wa watu hao walikuwa wakihitaji matibabu baada ya kukaa baharini karibu miezi mitatu bila maji wala chakula.
Mamlaka za Malaysia imesema kuwa haitaruhusu mashua hiyo kutia nanga katika ardhi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni