.

.

27 Juni 2015

BAVICHA BORA CHADEMA ICHELEWE KUINGIA IKULU KULIKO KUPELEKA VIONGOZI WENYE NIA YA KUJINUFAISHA.


Baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema limesema lipo tayari kuona Chadema inachelewa kuingia ikulu kuliko kupeleka ikulu viongozi wenye nia ya kujinufaisha na rasilimali za nchi zilizopo huku watanzania walio wengi wakiendelea kuteseka kwa maisha magumu.
Mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Patrobus Katambi ameyeyasema hayo wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Tarime mkoani Mara ambapo amesema Chadema kamwe haipo tayari kukimbilia ikulu kujinufaisha badala yake wapo tayari kuchelewa kuingia ikulu kwa kuwapeleka viongozi waadilifu wenye uchungu na taifa hili ambapo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Tarime Lukas Ngoto amesema Chadema haitasita kufanya maamuzi magumu kwa wanaotaka kukigawa chama hicho.
Nae mwenyekiti mstaafu wa Bavicha John Heche akizungumza na wananchi wa tarime baada ya kufanya maandamano makubwa kutoka Silali hadi Tarime ambapo amesema wakati sasa umefika kwa wananchi wa Tarime kufanya maamuzi magumu kuwapa ridhaa viongozi wenye uchungu na mateso ya wananchi wenye utayari wa kupigania rasilimali za Tarime zitumike kubadilisha maisha ya wananchi na sio kuendelea kunufaisha mikono ya watu wachache.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni