KINANA ATAHADHARISHA UJENZI WA GHOROFA.
KINANA ATAHADHARISHA UJENZI WA GHOROFA.
KATIBU Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amehadharisha Halmashauri ya
Manispaa ya Bukoba dhidi ya mpango wake wa kujenga soko la ghorofa kwa
kuitaka ijifunze kilichoikumba Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
baada ya kujenga soko la Machinga Complex .
Hadhari hiyo aliitoa
juzi katika mkutano wa hadhara katika eneo la Kashai, mjini Bukoba,
baada ya kupokea taarifa ya halmashauri hiyo juu ya mpango wake wa
ujenzi wa soko jipya la kisasa.
Kinana ambaye alihimiza watendaji kuhakikisha utekelezaji wa mpango wa
ujenzi wa masoko unakuwa shirikishi kuepuka migogoro na hasara, alisema
wafanyabiashara wana uwezo wa kushauri ni muundo gani wa soko unawezesha
kupata wateja. Baada ya kupokea taarifa hiyo ya halmashauri ikitaja
mpango wake wa kujenga soko la ghorofa, Kinana alisema, "Mimi sijawahi
kuona soko lenye ghorofa .
Nimezunguka nchi hii sana, Arusha, Tanga,
Dar es Salaam nenda pale Kariakoo hakuna ghorofa." "Kwa nini nasema
hivi? Kuna soko limeanzishwa Dar es Salaam linaitwa Machinga Complex,
lina ghorofa mpaka juu sasa wameshindwa kulipa kodi.
Kwa sababu,
nani yuko tayari kupanda ghorofa ya sita kwenda kununua chumvi...kwa
nini asinunue chumvi barabarani kwa hiyo jihadharini,"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni