Uzinduzi huo uemfanyika hapa Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya
wanchama wa chama hicho ambapo akizungumza na wageni hao na waandishi wa
habari Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni mgombea urais wa Zanzibar
kupitia chama hicho cha CUF amemsmea ilani hiyo imelenga kuwaptia
wazanzibari mabadilko si ya serikali pekee ila matumaini ya kuwa na nchi
yao yenye mamlaka kamili na neema kwa wote.
Katika ilani hiyo yenye kurasa 92 na vipengele 12 vinavyoelezea
mikakati mbalimbali ya kuongoza serikali na sera za uimarishaji sekta
mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, mazingira na uimarishaji wa haki za
binadamu na sekta za jamii huku mgombea huyo amemsmea hatua za maksudi
zitachukuliwa kuimarisha uchumi na maisha bora ya wannchi.
Mapema mwenyekiti wa kamti ya ushindi ya CUF ambaye pia ni waziri
wa biashara Mhe Nassor Ahmed Mazrui katika seriklai ya kitaifa
inayomaliza muda wake amesema CUF imepania kuwa na serikali yenye uwezo
mkubwa wa kuimarisha pato la serikali na seriklai itakuwa na uwezo
mkubwa wa kuzalisha ajira na kuleta wawekezaji watakaoleta tija kubwa
nchini.
Vuguvugu la kampeni za urais wa Zanzibar zimekuwa zikiendelea kwa
kasi na amani huku hadi sasa hakuna matokeo yeyote ya kuhatarisha amani
yaliyotokozea katika kampeni za urais wa Zanzibar ambapo kuna wagombea
14 wanawania nafasi hiyo ya kuongoza Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni