.

.

16 Januari 2016

TIMU YA TAIFA YA MIELEKA YA IRAN YATWAA KOMBE LA TAKHTI


Duru ya 36 ya mashindano ya kimataifa ya mieleka ya Kombe la Takhti imemalizika kwa timu ya taifa ya mieleka ya Iran kutwaa kikombe hicho.
Mashindano ya 36 ya kimataifa ya mieleka katika mtindo wa Greco-Roman na Freestyle ya Kombe la Takhti ilifanyika siku za Alkhamisi na Ijumaa katika Uwanja wa Ndani wa Azadi wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 12,000 hapa mjini Tehran. Iran ilionesha kuwa ni moto wa kuotea mbali katika mchezo huo baada ya kutwaa vikombe vyote viwili vya mashindano hayo katika mieleka ya mtindo wa Freestyle na Greco-Roman.
Timu ya taifa ya Iran ya mielea katika mtindo wa Freestyle imenyakua ubingwa baada ya kujikusanyia pointi 80 huku ndugu zao wa Greco-Roman wakiibuka kidedea baada ya kujizolea juma la alama 79.
Juma ya nchi 9 zilishiriki katika uga wa Greco-Roman huku wanamieleka kutoka nchi 13 wakichuana katika mtindo wa Freestyle.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni