.

.

26 Aprili 2016

MAADHIMISHO YA SIKU YA YWCA DUNIANI YALIYOFANYIKA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI MBEYA

 Maadhimisho ya YWCA Kanda ya Nyanda za juu kusini a,mbapo maandamano yalianzia stendi ya Mbeya Retco hadi ukumbi wa Parish.
 Vijana wa matarumbeta ambao ndio walikuwa waongozaji wa msafara wa YWCA Nyanda za juu kusini.
 Meza kuu katika maadhimisho ya YWCA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.
 Kabla ya maadhimisho hayo Rais wa YWCA TANZANIA Bi Rosemary Robert Mabagala alipata nafasi ya kutembelea kituo cha Amani kinachopatikana Nsalaga Uyole kinacholea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
   Rais wa YWCA Tanzania Bi  Rosemary Robert Mabagala akiwa na watoto wa kiyuo cha Amani Nsalaga Uyole Mbeya.

 
Hapa ni katika ukumbi parish mkoani Mbeya ambako  Aprili 24,2016 kumefanyika maadhimisho ya Siku ya Chama Cha Wanawake na Wasichana( Young Women's Christian Association- YWCA) duniani ambayo kwa kandaya nyanda kusiniyamefanyika mkoani Mbeya na kukutanisha wadau kutoka mikoa ya Iringa,Mbeya na Songwe.
Mgeni rasmi alikuwa Rosemary Robert Mabagala ambaye ni Rais wa YWCA Tanzania  . Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano kuanzia maeneo ya stendi ya Mbeya Retco na kupitia kito cha daladala cha Rufaa na mpaka katika ukumbi wa Prish Mbeya.

 YWCA ni shirika lisilo la kiserikali linatoa huduma kwa wanachama na wasio wanachama bila kujali utaifa,jinsia au imani ya mtu. Lengo la shirika hilo ni kuunganisha uongozi na sauti za wanawake na wasichana ili kujenga usawa wa kijinsia,kiuchumi,kudumisha amani na uhuru sambamba na kutunza mazingira ya ustawi wa jamii yote. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kidunia ni "Kuunda Ulimwengu Unaojumuisha Wote" huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kanda ya nyanda za juu kusini ikiwa ni "kwa upendo tumikianeni'


YWCA Tanzania ilianzishwamwaka 1959 ikiwa ni miongoni mwa nchi 125 duniani zinazounganishwa na World YWCA ambayo makao yake makuu yapo Geneva Uswis.

 Bi  Rosemary Robert Mabagala Alisema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka mwezi Aprili yakiwa na lengo la kujenga jamii yenye kuheshimu utu wa binadamu,kutetea na kulindaa haki,usawa na amani kwa wote


Huku lengo kuu ikiwa ni kupinga ukatili wa kijinsia,Washiriki wa maadhimisho hayo walisisitiza umuhimuwa jamii kuungana kwa pamoja ili kupiga vita mimba na ndoa za utotoni kwani janga kubwa sana katika Taifa la Tanzaniaambapo iliwezwa kutaja mikoa inayoongoza,mkoa wa Shinyanga ambao unaongoza kitaifa kwa asilimia 59 ukifuatiwa na mkoa wa Tabora na Mara.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni