.

.

14 Mei 2016

JKT MGAMBO V JKT RUVU: MECHI KALI ZAIDI VPL JUMAMOSI HII, MGAMBO WATASHUKA DARAJA?




Mgambo-JKT-ushindi

Kitendo cha kushindwa kuifunga JKT Ruvu katika mechi ya Jumamosi hii moja kwa moja kitamaanisha kuwa timu nyingine ya mkoa wa Tanga, JKT Mgambo itakuwa imeteremka daraja kuwafuata ‘ndugu zao’ Coastal Union ambayo tayari imeteremka daraja.
Pambano la hili litakalopigwa katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga lina umuhimu mkubwa kwa kila timu. Mgambo yenye pointi 24 baada ya kucheza game 28 inahitaji kushinda game zao zote mbili zilizobaki (dhidi ya JKT Ruvu na Azam FC) ili kufikisha alama 30 na kusubiri matokeo ya washindani wenzake katika vita ya kuepuka kushuka ili kujua hatma yao.
Ikiwa imeshinda michezo mitano tu msimu huu, Mgambo inaweza kushuka daraja kwa mara ya kwanza tangu walipopanda VPL msimu wa 2012/13. JKT Ruvu inahitaji walau pointi mbili katika game zao mbili za mwisho (dhidi ya Mgambo kisha Simba SC) ili kuwa na uhakika wa kubaki katika VPL msimu ujao.
Timu hiyo ya Pwani imekusanya alama 29 ambazo haziwezi kuwafanya wawe salama kwa sababu Kagera Sugar iliyo nafasi ya 14 (nafasi ya mwisho kabisa kwa timu za kushuka) yenyewe ina alama 25 huku wakiwa na michezo miwili mkononi, wakati African Sports ina wafuata kwa karibu ikiwa na alama 26 baada ya kucheza game 28 pia.
Sare itakuwa na maana kiasi kwa Ruvu lakini itakuwa na maana mbaya kwa Mgambo kwa kuwa watateremka daraja rasmi baada ya misimu yao minne katika ligi kuu. Hii ni mechi kali zaidi ya VPL siku ya Jumamosi ukitoa ile ya Ndanda SC v Yanga SC ambayo inatazamwa kama ‘mechi ya kuwakabidhi mabingwa wa ligi kombe lao.’

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni