Mwalimu wa Shule ya Msingi Tambaruka Kata ya Mkwamba wilayani Nkasi
mkoani Rukwa, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumsababishia
ujauzito mwanafunzi wake anayesoma darasa la tano katika shule hiyo.
Ofisa
wa Elimu ya Msingi Wilaya Nkasi, Missana Kwangulla alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema mtuhumiwa amekabidhiwa katika kituo cha polisi kwa
ajili ya hatua zaidi.
Kwangulla alisema anaandaa taarifa kuipeleka kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu tukio hilo kwa kuwa jambo hilo lipo chini yake.
Kaimu
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkwamba, Juvenally Mmanzi alisema jana kuwa,
ofisi yake ilipata malalamiko kutoka kwa mzazi wa mwanafunzi huyo.
Alisema
walichukua jukumu la kwenda kumpima mtoto huyo katika Zahanati ya
Mkwamba na kugundulika ni mjauzito wa miezi miwili na wiki moja.
“Baada
ya kujiridhisha tulianza kumhoji binti huyo na kumtaka amtaje mhusika
wa ujauzito huo, alimtaja mwalimu wake na kusema alikuwa katika
mahusiano naye ya kimapenzi tangu akiwa darasa la tatu,” alisema Mmanzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni