Waangola
kwa fitna wamo, maana tayari wameanza kuwavuruga Yanga mara tu baada ya
kutua kwenye uwanja wao wa ndege wa kimataifa mjijini Luanda.
Mara tu baada ya kutua, Yanga waligundua baadhi ya mizigo ya baadhi ya wachezaji ilikuwa imepotea.
Kazi ya kuanza kuitafuta ikaanza, haikuwa kazi rahisi na kukawa na mzozo mkubwa.
Katika hali ya kawaida ilionekana ni kama njia ya kuwachosha au kuwavuruga mpango ulioandaliwa mapema.
Hata
hivyo, ili kuwapa nafasi wachezaji wapumzike walilazimika kuwapandisha
ndege nyingine kwenye mji ambao klabu ya Esperanca ilipo ambako ni zaidi
ya kilomita 1200 kutoka Luanda.
Yanga
ambayo ilianza vizuri mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kwa
kuitwanga Esperanca kwa mabao 2-0 jijini Dar es Salaam, ilitua vizuri
katika mji huo.
Lakini
baadhi ya mashabiki na viongozi wengine walibaki Luanda wakisubiri
ndege nyingine huku wakitafuta mabegi ya wachezaji yaliyopotea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni