.

.

16 Julai 2016

MWENYEKITI UVCCM MBEYA AGUSWA NA MAISHA YA KIJANA EMANUEL FEDRICK ALIYEFUNGIWA NDANI MIAKA11


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mbeya Amani Kajuna akiwa amebeba kiti maalumu(Wheelchair) chenye thamani ya laki tatu na nusu (350,000) kwa ajili kumpatia msaada kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja jijini Mbeya ,ambaye aligundulika akiwa amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka 11 mara baada ya kuzaliwa akiwa na tatizo la ulemavu wa akili na viungo.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya (katikati )akiwa na baadhi ya wadau wakielekea mahala anapoishi kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja jijini Mbeya ambaye aligundulika akiwa amefungiwa ndani na wazazi wake kutokana na ulemavu wake kwa zaidi ya miaka 11 ,ambapo mwenyekiti huyo alitoa msaada wa kiti maalumu (wheelchair) pamoja na godoro na mahitaji mengine.

Nyumbani anakoishi kijana Emanuel Fedrick na wazazi wake mtaa wa Mwambenja Iganjo jijini Mbeya.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna akimtazama Kijana Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la ulemavu wa akili na viungo ambaye aligundulika akiwa amefichwa ndani na wazazi wake kutokana na tatizo lake ambapo aliishi ndani kwa zaidi ya miaka 11 bila kupata mahitaji muhimu ambapo aliwataka walezi wa kijana huyo kuhakikisha wanamtunza vyema kijana huyo nakuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki moja(100,000)kila mwezi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya Amani Kajuna akitoa maelekezo kwa wazazi wa kijana Emanuel Fedrick mara baada ya kukabidhi rasmi kiti maalum (Wheelchair)kwa kijana huyo .


Mama Mzazi wa kijana Emanuel Fedrick amwenyetatizo la ulemavu wa akili na viungo akipokea godoro ambalo limekabidhiwa na David Nyembe kwaniaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mbeya.
Muonekano halisi wa Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Iganzo Mbeya ambaye anatatizo la akili akiwa amelala .Picha E.Madafa,D.Nyembe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni