Jumatatu, Januari 25, 2016
Meneja wa
Manchester United Louis van Gaal, 64, anakaribia kujiuzulu baada ya
kukiri kuwa amewaangusha mashabiki (Sun), Van Gaal atakuwa na mazungumzo
na makamu mwenyekiti wa United Ed Woodard kujadili jinsi ya kukatisha
mkataba wake unaokwenda hadi mwaka 2017 (Star), Woodward amezungumza na
wachezaji wakuu wa United kuhusiana na mikakati ya Van Gaal na
anafikiria kumteua Ryan Giggs kuwa meneja hadi mwisho wa msimu (Mail),
meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, 52, anazidi kupata matumaini
ya kuwa meneja wa Manchester United (Times), meneja wa zamani wa
Tottenham Harry Redknapp anaamini Manchester United wangekuwa tayari
wamempa kazi Jose Morinho, kama wangekuwa wanamtaka, na anadhani
wanasubiri hadi mwisho wa msimu kujaribu kumchukua meneja wa Bayern
Munich, Pep Guardiola, 45, au Diego Simione, 45 kutoka Atletico Madrid
(Telegraph), Liverpool wamekubaliana maslahi binafsi na Shaktar Donetsk,
kumsajili mshambuliaji Alex teixeira, 26 (Futbol Ukraine), hata hivyo
bado hakuna muafaka juu ya ada wanayotaka kutoa Liverpool na bei
iliyowekwa kwa mchezaji huyo kutoka Brazil (Liverpool Echo), kiungo wa
Fiorentina Mario Suarez anafikiria kuhamia Watford (Mirror), Roma
wamethibitisha kuwa wanazungumza na Jiangtsu Suning ya China kuhusiana
na kumuuza mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho, 28 (Guardian),
mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Greizman, 24, amesema hana
mpango wa kuondoka Spain na kujiunga na Chelsea kwa pauni milioni 75
(Telefoot), Chelsea wamekuwa wakimalizia kukamilisha usajili wa
Alexandre Pato, 26, kutoka Corinthians kwa mkopo, huku wakitazamia
kumsajili moja kwa moja baadaye (Mail), Newcastle wamepunguza kasi ya
kumnyatia winga wa Tottenham Andros Townsend, 24 kutokana na Spurs
kutaka pauni milioni 14 (Sky Sports), Newcastle wanaonekana kufanikiwa
kubaki na kiungo kutoka Ufaransa, Moussa Sissoko, 26, lakini mchezaji
huyo amesema huenda akaondoka mwisho wa msimu (Sun), mshambuliaji wa
Liverpool Christian Benteke, 25, huenda akaondoka Anfield baada ya
michuano ya Euro 2016 (Bleacher Report), nahodha wa Manchester City,
Vincent Kompany, 29, anakabiliwa na jeraha jingine la msuli wa mguu na
huenda asicheze kwa mwezi mmoja zaidi (Star). Hayo ni baadhi ya
yaliyoandikwa kwenye magazeti ya leo Ulaya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni