Jumatatu, Januari 25, 2016
Kila mtu anajua
umuhimu wa kunywa maji, lakini wanajua kunywa maji wakati wa mchana tu
hawafahamu umuhimu wa kunywa maji wakati wa usiku, hasa kwa wazee
wanaopata magonjwa ya mishipa ya damu kwenye moyo au ubongo.
Takwimu
zinaonesha kuwa wazee wengi wanagunduliwa kupata kiharusi wakati wa
asubuhi, wataalamu wanaona chanzo chake ni ukosefu wa maji wakati wa
usiku. Ukosefu wa maji mwilini unaongeza uzito wa damu, na kusababisha
magonjwa ya mishipa ya damu kwenye moyo na ubongo.
Wazee wengi
hawapendi kwenda chooni wakati wa usiku, hivyo hawataki kunywa maji
kabla ya kulala. Kutokana na kibofu cha mkojo kutofanya kazi vizuri,
ukubwa wake unapungua, wingi wa mkojo unaongezeka na kusababisha ukosefu
wa maji mwilini. Hivyo kunywa maji wakati wa usiku ni muhimu kwa wazee.
Lakini kwa wazee wanao udhaifu wa moyo au upungufu wa uwezo wa moyo,
hawafai kunywa maji mengi kabla ya kulala, ama sivyo shinikizo la damu
litaongezeka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni