.

.

25 Januari 2016

RAIS MAGUFULI AWARUDISHA NYUMBANI MABALOZI 6, AWATIMUA MAIMU NA MADENI KIPANDE, AWAONYA WATUMISHI

Rais Magufuli ameamuru kurudi nyumbani mabalozi wawili haraka akiwemo Dr Batilda Buriani, Dr James Nsekela wa Italia na Peter Kalaghe wa Uingereza
Pia Mkurugenzi mkuu wa NIDA Bw Mwaimu amesimamishwa kazi kuanzia sasa.
Akitangaza hatua hiyo, Katibu mkuu kiongozi Ombeni sefue amesema Batilda na mabalozi wengine watano wamekuwa hawafanyi kazi kikamilifu ya kuiwakilisha nchi kama jinsi majukumu yao yanaavyoeleza.
Sefue amewataka mabalozi hao watatu kuondoka leo hii katika nchi waliko na kurudi Tanzania
Kuhusu Mwaimu, Sefue amesema yeye na vigogo wengine watatu wa NIDA wameaimamishwa kazi mara moja.
Aidha Rais Magufuli amemfukuza kazi Katibu Tawala mkoa wa Katavi Madeni Kipande kwa kushindwa kazi na Rais kutokuridhishwa na utendaji kazi wake.
Kipande aliteuliwa na JK kuwa katibu tawala Mkoa wa Katavi wiki moja kabla ya Magufuli Kuapishwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni