Mwenzenu jana nilikuwa na mjadala hapa nyumbani, na mada kuu ilikuwa ni juu ya namna nzuri ya kupata mwenza.
Dada
yangu mkubwa ndiye aliyeanzisha huo mjadala kwa kumuuliza mama kama ni
vyema mtu kutafutiwa mke au mume wa kuoa au kuolewa, au kila mtu anawajibika kujitafutia mwenyewe mwenza wake na kuanza maisha?
Mama
alikuwa na haya ya kusema. Alisema kuwa kimsingi hapo zamani wazazi
walikuwa wakiwatafutia watoto wao wenza wa kuoa au kuoelwa na lengo kuu
lilikuwa ni kutaka mtoto wao aangukie katika mikono salama na mojawapo
ya vigezo vikuu vilivyokuwa vikiangaliwa ilikuwa ni historia ya ukoo
husika, kwa mfano, je ukoo huo unaanguka kifafa? Je ni ukoo wa wachapa
kazi kwa maana ya kujituma kwa kufanya kzi kwa bidii ( Ikumbukwe kuwa
zamani kazi kuu ilikuwa ni kilimo). Je
Sio ukoo wenye mkono mrefu, yaani sio wezi ( Sijui kwa nyakati hizi
kuna haja pia ya kuwajumuisha na mafisadi yaani kama ukoo una hulka ya
ufisadi)
Jambo
lingine lilikuwa ni kuangalia kama ukoo unashambauliwa na magonjwa
sugu, kama vile anemia (Upungufu wa damu wa mara kwa mara) Kansa,
kisukari na maradhi mengine yaliyokuwa yakitafsiriwa kuwa yanaweza
kuushambulia ukoo.
Sina
hakika kama vigezo hivyo bado vinazingatiwa kwani kule vijijini bado
utaratibu a kutafutiana wenza upo lakini sio kwa kiwangom kama cha
zamani kwa sababu ya mabadiliko yaliyoikumba jamii, kwani kila mtu sasa
na lwake.
Kulizuka
hoja mbalimbali ambazo kama nikiziweka hapa nitawachosha, na lengo
langu ni kutaka kuwashirikisha wasomaji wa kibaraza hiki kisichoisha
visa na mikasa kutafakari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni