.
16 Septemba 2015
WAKIMBIZI WENGINE WAMEKIMBILIA ZIMBABWE
Kiongozi mmoja wa serikali nchini Zimbabwe ametangaza kuwa, raia wengine kadhaa wa Burundi wamekimbilia nchini humo kutokana na machafuko yanayoendelea nchini mwao. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zimbabwe, Davies Mwila na kuongeza kuwa, idadi ya Warundi waliokimbilia Zimbabwe kutokana na machafuko yaliyoibuka kuanzia mwezi April mwaka huu, imeongezeka na kufikia watu 570.
Waziri huyo wa Zimbabwe amesema kuwa hadi sasa ni Warundi 300 pekee waliowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Meheba, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Machafuko nchini Burundi yaliibuka mwezi April mwaka huu, baada ya wapinzani kumiminika mabarabarani kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa awamu ya tatu katika uchaguzi uliopita, machafuko ambayo yamefuatiwa na mauaji ya kuvizia ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana dhidi ya viongozi wa serikali na wale wa upinzani, na kuifanya hali ya mambo kuwa mbaya zaidi nchini humo.
Mbali na Zimbabwe, raia wengine wa Burundi wamekuwa wakimbizi nchini Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni