Serikali ya
Tanzania itaunda kitengo maalum cha kupambana na uwandaji haramu wa
wanyamapori, Profesa Abdallah Maghembe, waziri wa maliasili na utalii
alisema jana (Jumanne).
Hatua hiyo
inajiri wiki mbili baada ya wawindaji haramu kupiga risasi na kuangusha
ndege ya helicopter iliyokuwa ikipiga doria katika hifadhi ya Maswa,
kusini ya mbuga ya taifa ya Serengeti.
Hadi sasa watu tisa wametiwa mbaroni kuhusiana na kisa hicho ambapo rubani Roger Gower kutoka Uingereza aliuawa.
"Hii ni mojawapo
tu ya hatua ambazo zinachukuliwa na serikali ya Tanzania kuimarisha
vita dhidi ya uwindaji haramu na uporaji wa maliasili," Profesa Maghembe
alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni