Huduma ya
WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya
programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1.
Kampuni ya
Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia kustawisha
“huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”
WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016.
Licha ya kuacha
kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea
kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo
hutumia mfumo wa Android.
Kampuni hiyo
imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia
sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
- Android 2.1 and Android 2.2
- Blackberry OS 7 and earlier
- Blackberry 10
- Nokia S40
- Nokia Symbian S60
- Windows Phone 7.1
Kampuni hiyo
imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya
simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia."
Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni