Mapenzi hayapo ili yatutese, badala yake mapenzi yapo kwa ajili ya kutupa faraja.
Muondoe akilini mwako mtu wa aina hiyo, kwani atakufanya uyaone maisha kwa mtazamo hasi jambo ambalo siyo zuri.
NINI CHA KUFANYA?
Hili
ni swali ambalo kwa hakika linahitaji majibu yakinifu ili kuondoa vilio
vya mapenzi vinavyowakumba wengi, kama nilivyoeleza huko nyuma kuwa
mapenzi yana kanuni zake ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kuepusha
maumivu.
UAMINIFU NI MUHIMU
Ukiwa
mwaminifu katika ndoa au uhusiano wako, basi itakuwa ni vigumu kwako
kuteswa na mapenzi maana utakuwa umefuata moja ya kanuni zake.
Si
busara kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja ukidhani ni ujanja au ni kwenda na
wakati, la hasha, mapenzi hayaendi hivyo na usipokuwa makini utaishia
kulia kila mara.
Utakapobainika
kuwa wewe si mwaminifu, watu wengi watakutumia kimapenzi kwa faida zao
na mwisho watakuacha ungali bado unawahitaji na hapo ndipo mwanzo wa
chungu ya mapenzi huanza, yaani kuachwa na mtu ambaye bado unampenda.
Kwa waliowahi kutokewa na hali hiyo, wanaelewa ninachomaanisha. Acha kurundika wapenzi. Jiheshimu na mapenzi yatakuheshimu!
UONGO
Kudanganya ni sumu kwenye mapenzi, kama wewe ni mzuri wa kupiga porojo katika uhusiano wako, basi mapenzi ni lazima yakutese.
Kwa nini uwe muongo katika mapenzi? Jifunze kuwa mkweli na katika hali ya kawaida, huwezi kukwepa uongo kama huna uaminifu.
Leo uko na huyu, kesho uko na yule, maisha hayo hadi lini rafiki yangu? Utaishia kuwadanganya wanawake hadi lini?
Ikiwa wewe ni mwanamke, utawapanga wanaume hadi lini? Unadhani kuchuna mabwana ndiyo maisha yanaishia hapo?
Unapoteza muda wako mwingi katika kuhangaikia mapenzi, badala ya kuwaza mambo muhimu ya maendeleo.
Kama
una mpenzi au bado hujampata, basi vuta subira atakuja. Jambo moja
muhimu kuamini ni kuwa kila mmoja ana mwenza wake maishani, tatizo
linakuja pale tunapoishiwa na uvumilivu na badala yake tunageuka watu wa
kudandia na kubadilisha wapenzi kama nguo kila kukicha.
Hayo
siyo maisha jamani. Vuta subira, msubiri wako yuko njiani anakuja,
ikiwa umeshampata basi tulia naye huku mkipanga mikakati ya mafanikio
kwenye ulimwengu huu uliojaa ushindani.
Si
kwamba hawaruhusiwi kupenda la hasha! Nashauri waache kupaparukia
mapenzi kwa kutofuata kanuni zake. Yataishia kutuliza kila kukicha.
Mapenzi
yapo tangu enzi za mababu zetu, ya nini kuyaendea pupa? Epuka sana
kunga’ng’ania mapenzi kwa mtu asiye na chembe hata moja ya mapenzi juu
yako.
Kung’ang’ania
usipopendwa ni kujiletea mateso ambayo mimi nasema si ya lazima. Ndugu
yangu, wewe ni mzuri mno, mapenzi yasikuumize kabisa. Usiumie kwa
kumkosa wako wa maisha, inawezekana hajajitokeza tu!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni