MKURUGENZI WA KAMPUNI YA LUTANDULA'S
COMPANY LTD ALPHONCE MAGESSA ALIYESIMAMA AKITOA UFAFANUZI WA KEMIKALI
MPYA MBELE YA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA THABIT OLE MATEPET.
KAHAMA
Ofisi ya madini mkazi wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuzunguka katika maeneo ya machimbo ya wachimbaji wadogo ili kutoa elimu ya Matumizi ya Kemikali mpya ya kuchenjulia dhahabu ya Gold Dressing Agent (G.D.A).
Wito huo umetolewa mjini Kahama na Katibu tawala wa
wilaya Thabit ole Matepeti
aliyemuakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika Semina ya mafunzo ya matumizi ya
Kemikali hiyo iliyoandaliwa na
kampuni ya Lutandula’s Company Ltd kwa
wadau wa shughuli za madini wilayani Kahama.
Matepeti amesema kuwa wachimbaji wadogo wakipewa elimu
ya kutosha kuhusu matumizi ya Kemikali mpya ya kuchenjulia Dhahabu ya G.D.A
itasaidia kuinua vipato vyao,ikiwa ni pamoja na kuokoa afya zao na kulinda
mazingira kwa ujumla.
Akielezea umuhimu wa Kemikali hiyo Afisa madini Mkazi
wilayani Kahama Sophia Omary amesema kuwa licha ya kukamata dhahabu kwa haraka
mabaki ya kemikali hiyo ina uwezo wa kutumiaka kama mbolea tofauti na kemikali
zingine.
Kwa upande wake Afisa kutoka ofisi ya mkemia wa
Serikali kanda ya ziwa Rwige Ogunya amesema kuwa Kemikali ya G.D.A haina
madhara kama zilivyo kemikali ya Mercury na Cyanide
ambazo mara nyingi zimetajwa kusababisha madhara kwa binadamu,wanyama na
mazingira.
Naye mkurugenzi wa Kampuni ya Lutandula’s Companya Ltd
ambaye ndiye Msambazaji wa kemikali hiyo
barani Africa Alphonce Magessa amesema kuwa kemikali hiyo itasaidia kuinua
uchumi wa wachimbaji wadogo kutokana na uwezo wake wa kukamata dhahabu na
kuiiacha ikiwa na ubora wake asilia.
Sambamba na hayo Magessa ameongeza kuwa Lengo la
kuingiza kemikali hiyo nchini na barani Africa kwa ujumla ni kulinda usalama wa
wafanyakazi migodini pamoja na viumbe hai vinavyozunguka maeneo ya migodi.
Awali akielezea ubora wa kemikali hiyo Mshauri Mkuu wa
kampuni ya Lutandula’s Baraka Adroph amesema kuwa Kemikali hiyo aina viambata
vyenye madhara hali unayoweza kukaa nayo ndani na kuendelea na shughuli zozote
zile pasipo kuleta madhara.
Kemikali mpya ya Uchenjuaji Madini ya Gold Dressing
Agent (G.D.A) inayopataikana barani Africa kwa sasa inapatikana wilayani Kahama
kupitia kampuni ya Lutandula’s Company Ltd.
Kwa yeyeto anayehitaji Kemikali hii au anahitaji kujua
mengi kuhusu Kemikali hii Mpya wasilaiana na Mkurugenzi Kwa namaba
+255 765 245 514 au +255 28 2711111 au E-mail alphonce.magesa@lutcol.co.tz au
Bofya hapa kwa maelezo Zaidi http://lutcol.co.tz/
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA
LUTANDULA'S COMPANY LTD WAKIWA KATIKA SEMINA YA KUTAMBULISHA KEMIKALI
HIYO KWA WADAU WA MADINI.
BAADHI YA WANAFUNZI WALIOHITIMU MAFUNZO YA
MADINI KATIKA VYUO VYA MADINI VYA DODOMA NA SHINYANGA WAKIWA KATIKA
SEMINA YA KUTAMBULISHA KEMIKALI MPYA YA GOLD DRESSING AGENT (G.D.A)
BAADHI YA WADAU WA MASUALA YA MADINI WAKIWA
KATIKA SEMINA HIYO,WA KWANZA KUSHOTO NI MGENI KUTOKA NCHINI CHINA AMBAPO
KEMIKALI HIYO INATENGENEZWA.
MKURUGENZI WA KAMPUNI YA LUTANDULA'S MR MAGESSA AKITOA MAELEZO NAMNA ALIVYOANZA KUAGIZA KEMIKALI HIYO.
WADAU WA KAMPUNI YA LUTANDULA'S WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO.
MENEJA UFUNDI WA KAMPUNI YA LUTANDULA'S COMPANY LTD IDRISA MAFUMBI ALIYESIMAMA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA SEMINA HIYO.
MTAALAMU WA MASUALA YA UTUNZAJI KEMIKALI
KUTOKA KAMPUNI YA LUTANDULA'S AMANI MAGESSA ALIYESIMAMA AKIJITAMBULISHA
MBELE YA WANA SEMINA.
MHASIBU WA KAMPUNI LUTANDULA'S COMPANY LTD REMMYFRIDA MSWAHILI ALIYESIMAMA AKIJITAMBULISHA KATIKA SEMINA HIYO
INJINIA WA MADINI WA KAMPUNI YA LUTANDULA'S
COMPANY LTD FROLIAN MUTTA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA SEMINA YAMAFUNZO YA
MATUMIZI YA KEMIKALI MPYA YA GOLD DRESSING AGENT.
MMOJA WA WANAFUNZI WALIOHITIMU KATIKA CHUO
CHA MADINI DODOMA AKIULIZA SWALI YA NAMNA KEMIKALI YA GOLD DRESSING
AGENT (G.D.A) INAVYOFANYA KAZI.
AFISA MADINI MKAZI KUTOKA WILAYA YA KAHAMA
SOPHIA OMARY AKIELEZEA UMUHIMU WA KEMIKALI HIYO NA MIPANGO YA OFISI YAKE
KATIKA KUWAFIKIA WACHIMBAJI WADOGO NA KUWAPA ELIMUHIYO.
MSHAURI MKUU WA KAMPUNI YA LUTANDULA'S BARAKA ADROPH AKIELEZEA NAMNA KEMIKIALI YA G.D.A INAVYOTOFAUTIANA NA KEMIKALI NYINGINE.
BARAKA ADROPH AKIENDELEA NA UFAFANZI WA KEMIKALI HIYO.
KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA THABIT OLE
MATEPET AKIMPA MKONO WA HONGERA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA
LUTANDULA'S COMPANY LTD BWANA PHILIPO MAGESSA MARA BAADA YA KUFUNGUA
SEMINA HIYO.
AFISA KUTOKA OFISI YA MKEMIA KANDA YA ZIWA BWANA RWIGE OGUNYA AKITOA ELIMU KWA WANA SEMINA KATIKA UKUMBI WA NSSF MJINI KAHAMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni