Kwanza nashukuru kuitwa kwenye kikosi cha Stars, niliamini ipo siku nitaitwa kikubwa ni kuongeza juhudi pamoja na kujituma, tumefanya mazoezi mchana huu kwasababu ya kuzoea hali ya hewa ya Tanga, Tanga kuna joto na mara kadhaa huwa linatusumbua tukienda kucheza na timu za huko.
"Coastal wameshuka daraja lakini hatuwadharau, ni timu bora na tunataka kushinda mechi hiyo ili kuendelea ushindi na lengo letu ni kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, lengo hilo tuliliweka tangu awali kuwa tumalize ligi tukiwa kwenye nafasi hiyo," alisema Kakolanya
Prisons imekusanya pointi 48 ambapo Mtibwa Sugar wenyewe wana pointi 47 huku kila mmoja akimwombea mwenzake apoteze mechi ya mwisho ili aweze kujinyakulia kitita cha Sh 23 milioni.
Yanga ambao ni mabingwa wa VPL watajinyakulia Sh 81 milioni, mshindi wa pili atapataSh 40 milioni ambapo atakuwa kati ya Simba au Azam huku mshindi wa tatu atapewa Sh 29 milioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni