Waendesha
mashtaka nchini Ufaransa wanachunguza tuhuma za ngono kwa watoto
zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi wa nchi hiyo pindi walipokuwa katika
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wizara ya Ulinzi imesema itahitaji kutolewa kwa adhabu kali zaidi dhidi ya yeyote atakae patikana na hatia.
Mashtaka hayo
yamefunguliwa baada ya kupatikana kwa nyaraka zilizotolewa mwezi July na
mfanyakazi mwandamizi wa Umoja wa Mataifa.
Afisa huyo
alisimamishwa kazi baada ya kupewa nyaraka hizo za siri kwa Ufaransa.
Farhan Haq, msemaji msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki
Moon, amesema Umoja wa Mataifa umefanya uchunguzi wa tuhuma hizo, ambazo
itazifuatilia kwa kina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni