Tanzania Prisons wakiwa Mazoezini( Picha na David Nyembe wa Fahari New) |
Azam Fc wakiwa katika Mazoezi ( Picha na David Nyembe wa Fahari New) |
Joto
la mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu ya Tanzania Prisons ya
jijini Mbeya na timu ya soka ya Azam FC wenyeji wa Chamanzi jijini Dar es
Salaam itakayopigwa katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya siku ya
jumatano linazidi panda.
Timu ya Azam FC imesalia jijini Mbeya baada ya
mchezo wao wa kwanza na timu ya jiji ya Mbeya City ambao uliwapa Azam FC faida
ya pointi tatu muhimu baada ya kushinda goli 3 dhidi ya wenyeji wao Mbeya City.
Kuelekea
mchezo huo wa siku ya jumatano, kocha mkuu wa timu ya Azam FC Stewart John Hall
ametamba kwamba timu yake imejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi zote sita
kwa kuwapiga Tanzania Prisons katika uwanja wao wa nyumbani.
Upande wa wenyeji wa Azam FC, Tanzania Prisons
ambao wamewasili mkoani Mbeya jana wakitokea huko mkoani Tanga waliko toa suluhu
ya 1-1 na timu ya JKT Mgambo , kocha wa Tanzania Prisons Salum Mayanga wamesema
kuwa kutokana na uchovu wa safari wanaendelea na mazoezi ya kawaida ila
watahakikisha kuwa wanashinda mchezo huo .
Creadit Fahari News
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni