Rais Museveni
ametoa matamshi hayo baada ya Umoja wa Ulaya kukosoa jinsi zozei la
uchaguzi wa hivi karibuni nchini Uganda lilivyofanyika. Katika taarifa
yao waangalizi wa Umoja wa Ulaya walisema kuwa, chama tawala cha Rais
Yoweri Museveni cha NRM, kiliharibu mazingira ya uchaguzi kwa kuzua hofu
na wasiwasi dhidi ya viongozi wa upinzani na wafuasi wao. Aidha taarifa
hiyo ilibainisha kwamba, siku ya kufanyika uchaguzi huo mkuu vituo
vingi vya kupigia kura na hasa katika mji mkuu, Kampala, vilifunguliwa
kwa kuchelewa. Akijibu matamshi hayo ya Umoja wa Ulaya Rais Museveni
amesema hahitaji nasaha wala mahubiri ya Umoja wa Ulaya, kwani hawako
sahihi. Tume ya Uchaguzi ya Uganda juzi alasiri ilitangaza kuwa Yoweri
Museveni ni Rais Mpya wa nchi hiyo baada ya kushinda zaidi ya asilimia
60.8 huku mpinzani wake mkuu Kizza Besigye akipata asilimia 35.4. Hata
hivyo matokeo hayo yamelalamikiwa na wapinzani. Wakati huo huo, mgombea
wa FDC Kizza Besigye leo alitiwa tena mbaroni ikiwa ni mara ya nne
katika kipindi cha siku nane. Ingrid Turinawe, mmoja wa maafisa wa Chama
cha FDC amethibitisha habari ya kutiwa mbaroni Besigye na kubainisha
kwamba, vyombo vya usalama vinapaswa kumuachia huru mgombea wao huyo ili
apate nafasi ya kukusanya ushadidi unaothibitisha kwamba, uchaguzi
uliomrejesha madarakani Rais Museveni ulijaa wizi na udanganyifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni