.

.

25 Februari 2016

KWA NINI UJAZO WA BETRI ZA SIMU ZETU UNAPUNGUA SIKU HADI SIKU?


Betri za simu za mkononi huwa ni za Lithium. Ujazo wa betri ukipungua kwa theluthi moja, betri hiyo haiwezi kufanya kazi tena. Lakini hata kama hauitumia, bado itapoteza ujazo wa umeme baada ya miaka kadhaa. Na ukiitumia sana, huenda itaisha nguvu ndani ya miaka miwili tu.
Betri zinafanya kazi kutokana na mabadiliko ya kikemikali. Baada ya kutumiwa kwa muda fulani, kuhama kwa lithium ions ndani ya betri kutazuiliwa na kemikali nyingine hatua kwa hatua, mpaka betri itashindwa kufanya kazi tena.
Tunaweza kusema betri inafana na vitambaa tunavyotumia jikoni. Baada ya kusafishwa na kukaushwa kwa mara nyingi, vitambaa hivyo vinachakaa na mwishowe tunatakiwa kuvitupa.
Siku hizi bado hatuwezi kuzuia kupungua kwa ujazo wa betri, lakini hii haimaanishi kwamba hatuna teknolojia nzuri, bali wateja hawataki kununua betri za bei kubwa, hivyo watengenezaji wa betri wanatengeneza betri nyingi zenye ujazo mdogo na bei nafuu tu. Sababu nyingine ni kwamba kwa kawaida tunabadilisha simu za mkononi kila baada ya miaka miwili, hivyo haina haja ya kutengeneza betri zinazoweza kutumiwa kwa muda mrefu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni