Klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji
Manara amesema TFF kuendelea kufumbia macho kauli za kejeli, dharau, matusi na
kashfa zitolewazo na afisa habari wa klabu ya Yanga kutawafanya wao wachukue
hatua.
Manara amesema wakati alipokuwa kwenye mkutano
na waandishi wa habari akidai klabu ya Simba imechoshwa na kauli za Muro huku
TFF ikiendelea kubaki kimya.
“Mwishoni mwa mwaka jana msemaji wa Yanga
akiwa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, aliidhihaki klabu ya Simba na
viongozi wake kwa lugha za kashfa, kejeli, dharau na matusi. Alifikia mahali
anamwita makamu wa klabu ya Simba sanamu la michelini, mbaya zaidi alinikashfu
binafsi lakini kubwa alilikashfu kabila la Wazaramo”.
“TFF ikatoa kauli kwamba mwanzoni mwa mwaka
huu (January) itamchukulia hatua za kinidhamu kutokna na kauli zile, January
imepita, February inamalizika. Hatukusema kitu, baada ya mechi ya juzi mmesikia
kashfa zake na maneno yake”.
“TFF wako kimya, kesho Simba tukianza kusema
maneno ya kihuni watatuhukumu? Hayo mamlaka yatatoka wapi? Kama wanashindwa
kuchukua hatua kwa mtu anayetudhalilisha kila kukicha anajenga chuki na
uhasama”.
“Angalieni records, kamtukana mtu wa bodi ya
ligi, kamtukana makamu wa rais wa Simba, kamtukana Haji Manara, kaitukana ile
timu ya Kimondo, kila siku anatukana tu. TFF wasipochukua hatua Simba
tutachukua hatua sitishi litakalotokea tusilaumiane”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni